07 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Dereva mwingine Dar alizwa teksi
 
2008-05-07 19:44:22
Na Kiyao Hoza, Polisi Kati

Matukio ya uporwaji wa gari ndogo za abiria Jijini almaarufu kama teksi yameendelea kujiri ambapo jana usiku, dereva mmoja aliyekuwa amekodiwa na mwanamke alijikuta akiangua kilio baada ya kuporwa gari hiyo huku akishuhudia.

Taarifa za kipolisi zinasema waliofanya uporaji huo ni majambazi ambao walikuwa katika eneo la Goba na kutekeleza azma yao hiyo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jamal Rwambow, gari lililoporwa ni Toyota Corolla lenye namba za usajili T885 AGB.

Akasema gari hilo liliporwa saa 3:00 usiku katika baa moja inayojulikana kama Tree iliyopo Goba.

Akielezea tukio hilo, Kamanda Rwambow akasema kuwa mwanamke mmoja alikodi gari hilo katika kituo cha Taksi cha Ubungo akitaka kupelekwa Mbezi Samaki.

Akasema walipofika Mbezi Samaki, abiria huyo alipiga simu kwa mwenyeji wake.

Akasema baada ya hapo, abiria huyo alimtaka dereva ampeleke katika baa hiyo ya Tree.

Akasema walipofika hapo, akamueleza kuwa washuke ili akachukue malipo yake.

Kamanda huyo akasema dereva alitoka na kuliacha gari kwenda kuchukua malipo yake akiwa amefuatana na abiria wake.

Hata hivyo, wakati wakielekea kuchukua fedha, aliona gari lake likiendeshwa na mtu mwingine na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada ambazo hazikuzaa matunda.

Ajkasema kuwa hadi sasa, Polisi wanaendelea kumshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.