07 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere kutoa shahada za jinsia na maendeleo
 
2008-05-07 19:40:25
Na Adam Fungamwango, Jijini

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Nchini, kuanzia mwakani, kitaanza kutoa mafunzo kwa ngazi ya shahada ya kwanza ya masomo ya Jinsia na Maendeleo.

Akizungumza Jijini hivi karibuni, Mkuu wa Chuo hicho Dk. John Magoti, amesema kuwa chuo hicho kitakuwa ni cha kwanza nchini kutoa mafunzo katika kiwango cha shahada ya kwanza ya Jinsia na Maendeleo.

Amesema katika mafunzo hayo, yataonyesha tofauti ya kimaumbile au kibaiolojia kati ya mwanaume na mwanamke, ambapo, kila mmoja wao akizaliwa anabaki na tofauti hizo katika maisha yake yote.

Akifafanua zaidi, Dk. Magoti amesema kuwa, hata hivyo katika tofauti zao baadhi ya mifumo hufanana lakini mingine hutofautiana kama vile chakula na hewa ambavyo hufanana, lakini ni wanawake pekee ndiyo wana uwezo wa kubeba mimba na kujifungua na wanaume wana uwezo wa kupanda mbegu.

Dk. Magoti amesema kuwa lengo la kuanzisha mafunzo hayo, ni kuwapa wanafunzi ufahamu na uelewa zaidi kuhusu dhana na zana zihusizo Jinsia na Mendeleo katika nyanja za jamii, siasa na uchumi.

Alisema kuwa katika mafunzo hayo, wanafunzi akaendeleza ustadi katika kufanya utafiti wenye kuibua athari zitokanazo na kutokuwepo kwa usawa baina ya wanawake na wanaume katika kugawana na kutumia mali na raslimali.

Katika mikakati mingine, Dk Magoti alisema kuwa kuendelea uratibu wa kujiendeleza kwa wale ambao hawakupata bahati ya kuendelea na mfumo wa elimu ya kawaida, kuboresha vyuo vya elimu ya juu vilivyopo na kuwaendeleza kitaalam wanataaluma na wafanyakazi wasio wanataaluma.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.