|
Mama Dar afa baada ya kusombwa na gari
2008-05-06 16:11:12
Na Kiyao Hoza, Polisi Kati
Mama mwenda kwa miguu aliye mtu mzima wa miaka 61, Bi. Rozalia Lazaro, amefariki dunia jana baada ya kugongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara.
Tukio hilo limetokea Tabata, eneo la Segerea Magengeni Jijini.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Faustine Shilogile, ajali hiyo imetokea mishale ya saa 12:00 asubuhi.
Akasema gari lililomgonga marehemu lilikuwa likitokea Tabata Bima kuelekea Segerea.
Akasema mwanamke huyo alifariki papohapo na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Amana.
Akasema hadi sasa, Polisi wanaendelea kumsaka dereva aliyemgonga mwanamke huyo baada ya kuingia mtini na akipatikana, hatua zaidi za kisheria zitafuatia.
|