06 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Bunju B waaswa kushirikiana na TANESCO...
 
2008-05-06 16:10:31
Na Maabad Msuya, Bunju

Serikali imewapiga mkwara mzito baadhi ya wakazi wa Bunju B wanaoleta vikwazo katika zoezi linaloendelea la usambazaji wa umeme katika eneo hilo kwa kuwa hatua hiyo ni sawa na kupinga maendeleo yao wenyewe.

Mkwara huo umetolewa na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa katika eneo hilo, Bw. Siasa Samwel, wakati akizungumza na Alasiri kuzungumzia ujio wa umeme katika eneo hilo na changamoto wanazokabiliana nazo.

Mwenyekiti huyo amewataka wananchi wake kushirikiana na shirika la Umeme nchini, TANESCO badala ya kupinga kwa kuwa itakuwa ni sawa na kupinga maendeleo katika eneo lao.

``mradi huu ufamnikiwe... ni wazi kwamba baada ya hapo tutaweza kupiga hatua kubwa za maendeleo yatokanayo na uwepo wa nishati ya umeme,`` akasema Mwenyekiti huyo.

Kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita, Alasiri imeshuhudia mafundi wa shirika hilo ambapo walianza kwa zoezi la kuweka magogo na ndipo walipokutana na vipingamizi toka kwa baadhi ya wakazi.

Mwenyekiti huyo amelazimika kutoa wito huo kwa wananchi wake baada ya baadhi yao kuweka `ngumu` kwa Tanesco kupitisha nyaya katika maeneo yao, wakihofia kukatwa kwa minazi na miti yao ya matunda ikiwemo ya miembe na michungwa.

``Tunawaomba wananchi kushirikiana na shirika hilo kwani ujio wa umeme katika mtaa wetu ni neema kubwa ambayo tumekuwa tukiisubiri kwa muda mrefu... ni ndoto inayoelekea kuwa kweli. Tusijiharibie,`` akasema Mwenyekiti huyo.

Kutokana na tatizo la kukosa umeme katika eneo hilo kwa kipindi kirefu, baadhi ya wananchi wa eneo hilo walianza kuilalamikia Tanesco kwa ukimya wao na wengine kuanza kuhusisha kuwa kuna mkono wa kisiasa katika urtekelezaji wa jambo hilo.

Wananchi hao, awali walidai wanashangazwa mtaa wao ambao unaongozwa na chama pinzani kukosa umeme huku mtaa wa jirani wa Bunju A ambao upo chini ya CCM ukiwa unang\'ara kwa kupata umeme kila kukicha.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.