06 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Waziri Wassira ataka Hospitali ya Amana iwe na vituo vya afya
 
2008-05-06 16:05:07
Na Haji Mbaruku, Amana

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Stephen Wassira, ameitaka Hospitali ya Amana kujenga vituo vingine vya afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo.

Waziri Wassira ameyasema hayo baada ya kubaini kuwa hospitali hiyo hivi sasa imekuwa ikipokea wagonjwa wengi kuliko uwezo wake na hivyo baadhi ya wagonjwa kushindwa kupata huduma.

Waziri huyo alikuwa akizungumza na uongozi wa hospitali hiyo wakati alipotembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa mahala hapo.

Akasema Waziri Wassira kuwa vituo vya afya vinasaidia sana kutoa huduma kwa wagonjwa na hivyo ni bora vikaanzishwa ili kupunguza tatizo la mrundikano wa wagonjwa hospitalini hapo.

Akasema kuwa hivi sasa, wagonjwa wengi wanakimbilia hospitalini hapo kutokana na ukosefu wa vituo vingine vya afya.

Naomba muwe na vituo vya afya ili visaidie kupunguza tatizo la msongamano wa wagonjwa, akasema Waziri huyo.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa tatizo kama hilo lipo pia kwenye hospitali za Mwananyamala na Temeke, ambapo msongamano wa wagonjwa umekuwa mkubwa kulinganisha na uwezo wa hospitali hizo.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia baadhi ya wagonjwa katika hospitali hizo wakiendelea kulala wawili katika kitanda kimoja na kuhatarisha afya za wagonjwa hao.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.