05 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ajali Dar zaua wawili
 
2008-05-05 18:31:49
Na Kiyao Hoza, Polisi Kati

Watu wawili wamefariki dunia na mwingine kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti ya ajali zilizotokea Jijini leo na jana.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema tukio la kwanza limejiri leo, mishale ya 12:30 alfajiri, pale katika barabara ya Nyerere kunako njia panda ya Kiwalani.

Amesema tukio hilo limehusisha magari yenye namba za usajili T 885 ARN aina ya Mitsubishi Fuso iliyokuwa ikiendeshwa na Rahimu Kabuye, 23 na gari namba T 500 ABA aina ya Nissan Pick-Up iliyokuwa ikiendeshwa na Dashi Kasela, 50.

Amesema ajali hiyo imetokea wakati lori aina ya Fuso lilipopunguza mwendo na kuingia katika barabara ya Kiwalani.

Akasema hapo ndipo pick up hiyo ilipoigonga kwa nyuma.

Kamanda Shilogile amesema abiria aliyekuwa katika pick up, anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25-30, alitupwa nje ya gari kupitia kwenye kioo cha mbele na kujibamiza katika lori la Fuso na kufariki papohapo.

Amesema dereva wa gari hiyo amelazwa katika hospitali ya Amana na hali yake ni mbaya.

Aidha, amesema maiti ya mtu huyo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Amana.

Katika tukio jingine, mtoto Rose Fred, 6, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Nyerere, jana mishale ya saa 8:00 mchana.

Kamanda Shilogile amesema mwenda kwa miguu huyo aligongwa na gari lenye namba T 928 AAY Toyota Corolla iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika.

Amesema mwili wa marehemu umefadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Amana na dereva na gari lake wanaendelea kusakwa na polisi.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.