18 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Polisi Jijini wazungumzia kisa cha mtoto...
 
2008-03-18 15:27:48
Na Mwanaidi Swedi ,Jijini

Lile sakata la mtoto anayedai kudondoshwa na ungo wakati akiwa kazini na wenzake kwenye mambo ya kishirikina, polisi wamelitolea ufafanuzi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Jamal Rwambow, amesema taarifa hizo siyo za kweli na kwamba mtoto huyo anafanya utapeli kwa kutumia uongo huo.

Amesema siyo mara ya kwanza kwa mtoto huyo kuripotiwa kuwa amedondoka akiwa kazini na wenzake kwa shughuli za kishirikina.

Kamanda Rwambow amesema huo ni ujanja tu wa mtoto huyo na kwamba hakuna ukweli wowote dhidi ya kile anachokieleza.

Akizungumzia mazingira tofauti ya mtoto huyo, Kamadna amesema mnamo Januari 6 mwaka huu, majira ya saa 9:00 usiku mtoto huyo aliripotiwa kuwa alidondoka maeneo ya Kanisa la Kilutheri kule Tanki Bovu jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa alipookotwa eneo hilo la kanisa, alijitambulisha kwa jina la Nurudi Selema na kujifanya hawezi kuongea, hali iliyosababisha apelekwe kituo cha Polisi Kawe.

Hata hivyo alidai kuwa anahitaji huduma za kiroho ambapo aliombewa na kisha kupelekwa Hospitali ya Mwananyala ili kufanyiwa uchunguzi wa akili zaidi.

Aidha Kamanda amesema baada ya kufanyiwa uchunguzi walibaini kuwa mtoto huyo hakuwa na matatizo ya akili na akawa anapatiwa huduma mbalimbali ikiwemo chakula. Hata hivyo alitoroka.

Akaeleza kuwa baadaye mtoto huyo alibainika kuwa mwishoni mwa mwaka alionekana tena huko Tumbi hospitali akidai kuwa alianguka maeneo ya Kimara.

Alichukuliwa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Bw. Msuya kwa maombezi ya kiroho. Hata hivyo mtoto huyo inadaiwa alimuibia Bw. Msuya vitu mbalimbali na kisha akaingia mitini.

Kamanda amesema cha ajabu mtoto huyo ameripotiwa kudondoka tena na ungo maeneo ya Manzese na safari hii akitumia jina la Ramadhani.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.