28 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kiwango cha uzalishaji taka Soko la Kariakoo chapungua
 
2008-02-28 17:35:08
Na Grace Chilongola, PST- Jijini

Uzalishaji wa taka katika Soko la Kariakoo Jijini umepungua kutoka wastani wa tani 20 kwa siku hadi kufikia wastani wa tani 10 kwa siku.

Unafuu wa uzalishaji wa taka sokoni hapo umetokana na zoezi la kuondolewa kwa wamachinga, ambalo lilifanywa na manispaa ya Ilala mwezi uliopita.

Katika mahojiano yake na PST, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bw. Kuboja Ng’ungu, amesema kuondolewa kwa `machinga’` hao kumewafanya wawe na punguzo kubwa la uzalishaji wa taka.

Amesema zoezi hilo limesaidia kuondoa msongamono uliokuwepo sokoni hapo, ambao ulisababisha kuwepo kwa hewa nzito.

Bw. Ng’ungu anasema kupungua kwa uzalishaji wa taka kumesaidia kupunguza gharama za usafi kutoka zaidi shilingi milioni 13 kwa mwezi na sasa kufikia shilingi 6,180,000.

Amesema kuondoka kwa wamachinga kumeruhusu kuwepo kwa mzunguko mzuri wa hewa katika eneo la shimoni hivyo kuondoa kero ya joto na hewa nzito iliyotokana na kitendo cha wafanyabiashara hao kuziba vidirisha vya hewa kwa kufanyia biashara zao maeneo hayo.

Aidha, Bw. Ng`ungu amesema kuwa licha ya mapato kupungua kwa kiasi fulani, faida nyingine walizopata baada ya zoezi la kuwaondoa wamachinga kukamilika ni kuongezeka kwa usalama wa mali na wateja wao wanaofuata bidhaa mbalimbali sokoni hapo.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.