28 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kandoro apiga marufuku uuzaji hovyo wa pombe
 
2008-02-28 17:33:53
Na Moshi Lusonzo, Jijini

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Bw. Abbas Kandoro, amepiga marufuku uuzaji wa pombe katika glosari, hasa nyakati za usiku.

Mkuu huyo ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Awali, aliyeanza kuchokonoa suala hilo ni Diwani wa Kata ya Miburani, Bw. Fortunatus Mangw`ela.

Diwani huyo alitaka kujua mmiliki wa glosari iliyopo eneo la bustani ya Tazara, amepata wapi ujasiri wa kuuza vilevi nyakati za jioni huku leseni yake ikionyesha kuwa ameomba kuendesha glosari.

``Mheshimiwa Mwenyekiti... nataka kujua yule mmiliki wa glosari ya Tazara, amempa nani ruksa ya kuuza bia wakati yeye ameomba leseni ya glosari?,`` aliuliza Bw. Fortunatus.

Akijibu swali hilo,Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw. Idd Nyundo, akasema kuwa, iwapo mmiliki wa glosari hiyo anauza pombe kama anavyodai diwani Fortunatus, atakuwa anafanya makosa kwa sababu anapingana na sheria zilizopo.

``Kama anafanya hivyo, anavunja sheria... tutamsimamisha,`` akasema Bw. Nyundo.

Baada ya Mkurugenzi kutoa majibu hayo, ndipo Bw. Kandoro aliposimama na kutoia mchango wake kwa kusema kuwa, glosari zote zinazouza pombe Jijini zinakiuka Sheria ya Vileo ya mwaka 1958.

Akasema sheria hiyo inakiukwa na wengi kwa sababu hivi sasa, glosari nyingi Jijini zinauza pombe na nyingine huwaweka wateja wao barabarani na kuzuia wananchi wengine kuzitumia.

Akasema mbaya zaidi, hivi sasa kuna maduka ya kawaida ya vyakula na bidhaa nyinginezo yamegeukia uuzaji wa pombe, kinyume na sheria.``Sasa imekuwa kama hakuna viongozi... uvunjaji sheria hii umekithiri Jijini. Sasa viongozi lazima mkemee kivitendo uvunjaji huu wa sheria,`` akasema Bw. Kandoro.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.