28 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Korogwe wapigwa tafu
 
2008-02-28 17:32:47
Na Azizi Issa

Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 68 kwa wakazi wa vijiji tisa wilayani Korogwe.

Fedha hizo ni kwa ajili kuboresha utekelezaji miradi midogo ya kijamii na vikundi vya uzalishaji mali.

Kwa mujibu wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bw. Mweta Njema, pesa hizo zitatumika katika kuboresha miradi ya kilimo bora cha maharage, ufugaji kuku wa asili, mbuzi wa maziwa, matumizi ya wanyama kazi na kuhifadhi mazingira.

Akasema vijiji hivyo vilipewa pesa hizo Februari 2 mwaka huu wakati Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein alipofanya ziara mkoani humo.

Akasema miradi hiyo ni ya uboreshaji kuku asili, hifadhi ya mazingira na ufugaji wa mbuzi wa maziwa utafanyika katika vijiji vya Kwakibomi, Gombero, Magundi na Mgila.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.