27 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakati ufisadi ukipamba moto, bosi wa shirika la Fedha la Kimataifa kutua Bongo kesho
 
2008-02-27 17:24:46
Na Sharon Sauwa, Mikocheni

Huku sakata la ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) likiendelea kunguruma, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Fedha Kimataifa, (IMF), Bwana Dominique Strauss Kahn, anatarajiwa kuwasili nchini kesho.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Hazina, Bw. Gray Mgonja, lengo la ziara hiyo ya kikazi ni kubadilishana mawazo na viongozi hao kuhusiana na hali ya uchumi kwa ujumla.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Uchumi, imesema mkurugenzi huyo, atatanguliwa na wakurugenzi wa bodi wa shirika hilo wanaowakilisha nchi mbalimbali.

Taarifa hiyo imesema mkurugenzi huyo atapata nafasi ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar Abeid Karume na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pia ujumbe huo utafanya mazungumzo na gavana mpya wa BoT, Profesa Benno Ndulu na viongozi wengine na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

Mkurugenzi huyo anakuja nchini huku kukiwa BoT ikiwa inakabiliwa na kashfa nzito ya mapesa kibao ya akaunti ya nje (EPA) kuyeyuka kimiujiza.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.