|
PSI kuwasomesha wanafunzi watatu wa Jangwani sekondari
2007-10-25 16:26:54
Na Renatha Msungu, Jijini
Shirika la kuhudumia afya kwa jamii ambalo , PSI limetoa msaada wa kuwasomesha wanafunzi wanne wa shule ya Sekondari ya Jangwani walioshinda katika shindano la kuchora picha za kupiga vita gonjwa hatari la Ukimwi.
Picha hizo zimebandikwa katika ukuta wa shule hiyo, zinaelimisha kuhisiana na ugonjwa huo ambao umeenea kwa kiasi kikubwa.
Baadhi ya wanafunzi waliopata ofa hiyo ni pamoja na Beatrice John, Upendo Shamana, na Jackline Paul.
Kwa mujibu wa taarifa ya PSI, ofa waliyopewa wanafunzi hao ni pamoja na kusomeshwa miaka miwili shuleni hapo kwa mshindi wa kwanza huku mshindi wa pili akipewa zawadi ya kulipiwa ada ya mwaka mmoja wakati wa tatu atalipiwa ada ya nusu mwaka.
Mbali na zawadi hizo, pia Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Shule za Sekondari, Bw. Dickson Ndabise aliwakabidhi vyeti pamoja na risiti za ada kutoka kwa PSI.
Naye Mkuu wa Shule hiyo, Nancy Mabula, aliwaomba PSI wawaongezee vibanda kwa ajili ya wanafuzni kujisomea baada ya kutoka madarasani mwao.
`PSI walitujengea vibanda viwili, tunaomba watuongezee vingine ikiwezekana,` akasema Bi. Nancy.
Wakati huo huo, Bw. Mabula aliwataka PSI kuendeleza zoezi hilo katika shule mbalimbali za mchanganyiko.
`Hii inapendeza kwakweli... wanafunzi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu ukimwi. Kwa sababu hiyo, ni vyema PSI wakafanya zoezi hili pia katika shule zenye mchanganyiko wa jinsia,` akasema Bw. Ndabise.
Aliongeza kusema kwa upande wa Jangwani zoezi hilo.
|