25 Oct 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Tatizo la maji Kijiji cha Kyejo Mbeya kubaki historia
 
2007-10-25 16:18:38
Na Sharon Sauwa, Jijini

Wakazi wa Kyejo mkoani Mbeya watanufaika na mradi mkubwa wa maji utakaogharamiwa na kampuni ya nishati ya hewa ya oksijeni nchini, TOL na hivyo kulifanya tatizo hilo kubaki kuwa historia kwa wakazi hao.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Arnold Kilewo, amesema mradi huo utatekelezwa mwakani.

Akasema licha ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo, kampuni hiyo imejenga zahanati, shule na nyumba za walimu mbili katika kijiji hicho.

`Wananchi wa Kyejo wamekuwa wakipata maji kutoka katika kiwanda chetu hivi sasa huu mradi tutautekeleza katika kijiji cha jirani mwakani,` akasema.

Akasema miradi hiyo, ni utaratibu wa uliopangwa na kampuni hiyo wakurejesha walichokipata kwa wananchi.

Aidha, akasema wanahisa wa kampuni hiyo wataanza kunufaika na gawio la hisa mwakani mara baada ya kampuni hiyo kupata faida.

Akasema kampuni hiyo ilipata faida ya sh. 733,608,000 katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.

`Tumelipa madeni yote tuliyokuwa tukidaiwa...mara baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa mahesabu tutafahamu gawio litakuwa ni kiasi gani,` akasema.

Akasema faida hiyo ambayo bado haijakatwa kodi ni mara sita ya faida iliyopatikana mwaka jana.

Akasema katika kipindi cha mwaka mzima wa 2006, kampuni hiyo ilipata faida ya sh. 102,278,000.

Mkurugenzi huyo akasema mauzo ya kampuni hiyo yalipanda na kufikia sh. bilioni 4.087 katika miezi tisa iliyopita ukilinganisha na mwaka jana ambapo mauzo yalikuwa ni sh. bilioni 4,319.

Akasema miongoni mwa wateja wa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo ni makampuni ya vyuma, karakana, sekta ya madini, kilimo, viwanda vya usindikaji, vinywaji baridi na bia, hospitali na klinic.

Akasema kampuni hiyo imeanza kusafirisha na kuuza gesi katika nchi za Kenya, Zambia na Malawi.

Aidha, akasema kampuni hiyo iko katika hatua za kupata nembo ya ubora wa viwango ulimwenguni, ISO.
Kiwanda hicho kinazalisha gesi za Oksijeni, Nitrogen, Carbon Dioxide na Dissolved Acetylene.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.