03 May 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Zungu la unga laanika siri
 
2007-05-03 18:03:15
Na Sharon Sauwa, Jijini

Siku chache tu baada ya kunyakwa, zungu moja la unga limejikuta likianika siri moja baada ya nyingine kwa Jeshi la Polisi nchini na hivyo kutoa mwanga mpya katika mapambano dhidi ya biashara `kichaa` ya dawa za kulevya nchini.

Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, `zungu` hilo limeshamwaga siri kibao kubumbuluka, mojawapo ikiwa ni ile ya hati za kusafiria.

Zimesema taarifa hizo kuwa mtuhumiwa huyo waliyemnasa hivi majuzi na kujitaja kwa jina la Mtemi Kwimba, ndiye aliyewafumbua macho kwa kubaini kuwa kumbe, wafanyabiashara wa dawa hizo hutumia hati `feki` za kusafiria.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Madawa ya Kulevya, Bw. Nzowa, mtuhumiwa huyo aliyekuwa na hati ya kusafiria iliyoandikwa jina la Mtemi Kwimba, alibandika picha yake katika hati ya mtu mwingine huku jina lake halisi likiwa ni Mohamed Willy na sio lile linaloonekana.

``Wakati wa mahojiano alitueleza kuwa alibandika picha yake katika hati ya mwenzake,`` akasema Kamanda huyo.

Akasema wakati akielekea nchini India alitumia jina la Hussein Abubakar Ally na alipokuwa akirejea nchini alitumia jina hilo la Mtemi Kwimba.

Akasema watuhumiwa wengine wanaohusika na kugushi hati hizo wanatafutwa na polisi.

Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Mabawa mkoani Tanga alinaswa na pipi 27, saa 10.00 jioni Aprili 29 mwaka huu.

Kamanda Nzowa akasema, thamani ya dawa hizo ni zaidi ya Sh. Milioni Nane.

Akasema kukamatwa kwa mtu huyo kulifuatia kushukiwa kuwa alikuwa amebeba madawa hayo ya kulevya.

Akieleza zaidi, Kamanda Nzowa akasema mtuhumiwa huyo aliondoka nchini Machi 7 mwaka huu akitokea Tanga.

Awali, alipitia Hororo, akatua Nairobi nchini Kenya, akaenda Dubai na hatimaye akafika huko India kabla ya kunaswa wakati akirejea na mzigo Bongo.

  • SOURCE: Alasiri
Tuma Maoni Yako
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.