03 May 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Jibwa kichaa laibuka, latesa watu Jijini
 
2007-05-03 17:58:44
Na Zawadi Kapambwe, Kimara

Mbwa mmoja anayedhaniwa kichaa ameibuka kinamna na kuwatesa watu kwa kuwang`ata hovyo pale Kimara Jijini.

Hadi sasa, imeelezwa kuwa zaidi ya watu watatu wameshang\'atwa na mbwa huyo, lakini wote hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

Mmoja kati ya watu hao ametambuliwa kwa jina la Kulwa Sadick, 18, mkazi wa Kimara-Tanesco Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimara-Matangini, Bw. Sheby Mtambo, amesema watu hao walitafunwa na mbwa katika matukio tofauti kwenye maeneo ya Kimara-Tanesco na Kimara-Mahakamani.

``Tukio la kwanza lilitokea majira ya usiku ambapo mbwa aliwavamia watu waliokua wamekaa nyumbani kwao saa mbili za usiku na kumng\'ata Bw. Sadick mkono wa kushoto, `` akasema Bw.Mtambo.

Amesema baada ya tukio hilo, Bw.Sadick alikimbiziwa hospitali ambapo alitibiwa na kuruhusiwa.

Bw. Mtambo amesema katika tukio la pili, mbwa huyo aliwang`ata wanafunzi wawili wakati wanakwenda shuleni huko Kimara-Baruti.

Amesema baada ya kuwang\'ata wanafunzi hao wananchi walianzisha msako na kufanikiwa kumuua mbwa huyo.

Haikuweza kufahamika mapema iwapo mbwa aliyewauma watu hao alikuwa amepata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

Lakini idara ya mifugo katika kata ya Kimara, imeandika barua ya kumuita mmiliki wa mbwa huyo ili akaeleze undani wa tukio hilo.

Hata hivyo, barua hiyo ambayo Alasiri ilipata nakala yake, haikueleza kama mwenye mbwa huyo atachukuliwa hatua gani baada ya hapo.





  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.