02 May 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wadau walalamikia ukosefu wa taarifa za soko la mifugo nchini
 
2007-05-02 18:03:25
Na Futuna Seleman, Jiji

Imeelezwa kuwa ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu masoko ya mifugo ni moja kati ya vikwazo vikubwa katika kuwezesha uzalishaji wenye tija katika sekta hiyo nchini.

Hayo yamo katika hotuba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw. Said Kalembo, wakati akifunga semina ya wakusanya taarifa za masoko ya mifugo na bidhaa zake.

Hotuba hiyo imetolewa na Afisa Masoko wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bw. Julian Gutta, kufuatia semina ya siku mbili iliyofanyika mjini Morogoro hivi karibuni.

Akasema taarifa na takiwmu za masoko zitawezesha wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kufanya maamuzi yenye busara kuhusu maendeleo ya shughuli zao.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo, Bw.Kalembo akasema kuwa, wizara ya viwanda, biashara na amsoko pamoja na wizara ya maendeleo ya mifugo zinatambua mchango wa mfumo wa ukusanyaji, uchambuaji wa taarifa za masoko ya mazao ya kilimo hususan mifugo katika sekta nzima ya kilimo nchini.

Aidha, akasema mazingira ya ufugaji wa mfumo wa asili uanoutumiwa na wafugaji wengi nchini, unachangia kuwepo kwa pato dogo, wafugaji kuhamahama mar akwa mara kutafuta malisho na maji ikiwa ni moja ya sababu hizo.

Kadhalika, akawataka washiriki wa semina hiyo, kutafakari na kujadili mbinu za kuimarisha ubora wa taarifa za masoko ili ziweze kuwa za manufaa makubwa kwa wadau wanaozitumia.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.