01 May 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Manispaa Temeke yacharukia upandaji miti
 
2007-05-01 17:28:49
Na Futuna Seleman,Temeke

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam, inatarajia kupanda miti milioni 1.5 katika kata zake 24 zilizopo katika manispaa hiyo.

Akizungumza na Alasiri kuhusu mikakati ya uboreshaji mazingira, Ofisa Uhusiano wa manispaa hiyo, Bi. Joyce Msumba, amesema miti hiyo itapandwa katika kipindi cha kati ya mwaka huu na mwakani.

Akasema miti wanayotarajia kuipanda ni ya matunda, kivuli, kuni, mbao, mapambo na miti ya kuhifadhi vyanzo vya maji.

Akasema miti hiyo itapandwa maeneo ya wazi, makazi ya watu, mabondeni na katika fukwe za bahari na vyanzo vya maji.

Bi. Joyce akasema miti hiyo itapandwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utunzaji wa mazingira, zikiwemo asasi za Paees, Cross Road Garden, Jema, Celdec, Ketsone, Tampa na Youth Vision.

Akasema kuanzia mwaka 2000 hadi Desemba 2006, manispaa hiyo ilishapanda miti 4,325,789 katika maeneo ya wazi, makazi ya watu, mabonde, shamba la miti la manispaa, fukwe za bahari, shule na vyanzo vya maji.

Akasema kati ya mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu, wamefanikiwa kupanda zaidi ya miti 500,000.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.