01 May 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

CCM Dar waanza kutimuliana vumbi
 
2007-05-01 17:26:15
Na Badru Kimwaga, Kinondoni

Kitimtim cha uchaguzi wa ngazi mbalimbali katika chama tawala, CCM kimeanza kwa kishindo Jijini Dar ambapo baadhi ya watu wameshaanza kucheka kwa kuibuka videdea huku wengine wakiambulia patupu.

Kinondoni, kitimtim hicho kimeanza kwa mwanamama Amina Mleche kufanikiwa kuukwaa uenyekiti wa CCM-tawi la Muyebeya, Kata ya Kinondoni baada ya kuwabwaga wagombea wengine wawili.

Bi. Mleche alifanikiwa kutwaa ushindi huo kwenye uchaguzi wa tawi hilo uliofanyika katika tawi la Mkunguni eneo la Kinondoni.

Mwanamama huyo alipata kura 94 na kumbwaga aliyekuwa akiitetea nafasi hiyo, Bw. Said N. Matata aliyepata kura 40.

Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, alikuwa ni Bw. Zubeir Jumbe Shaweji ambaye aliambulia kura 13 tu.

Katika nafasi ya ukatibu mkuu, Bi. Sikitiko Mohammed alimbwaga Bw. Aziz Mrope baada ya kupata kura 26 dhidi ya 15 alizozipata mpinzani wake huyo.

Bw. Issa Mtaula aliula baada ya kunyakua nafasi ya Ujumbe wa Wilayakwa kupata kura 96.

Bw. Mtaula aliwabwaga Said Ngawina aliyepata kura 40 na Juma Namkuta aliyeambulia kura sita tu, huku kura nyingine tatu zikiharibika.

Naye Bw. Ally Lumeso alifanikiwa kuchaguliwa kuwa katibu mwenezi wa tawi hilo kwa kupata kura 27 akimbwaga Bw. Pascal Njige aliyeambulia kura 14.

Nafasi ya ujumbe wa kamati ya uchumi na mipango imeenda kwa Bi. Christina Madono aliyekuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo ambaye alipigiwa kura za ndio 41.

Akihutubia baada ya kuchaguliwa, Bi. Mleche akaomba ushirikiano kwa wanachama, viongozi wenzake katika kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama hicho inatekelezwa.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.