|
Wauza vito vya bahari walilia kozi za Kiingereza
2007-05-01 17:24:22
Na Jacqueline Mosha, Kivukoni Feri
Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Makombe wa Jijini Dar es Salaam, DDSS, Bw. Wales Chinunda, amesema wanatamani kuiomba Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuwasaidia mafunzo ya lugha za kigeni ili kurahisisha mawasiliano pindi watalii kutoka nje ya nchi wanapowaendea kwa nia ya kuulizia bidhaa wanazouza sokoni hapo.
Bw. Wales amesema kutozifahamu lugha mbalimbali za kigeni limekuwa tatizo kubwa na la kudumu kwao hasa wanapotembelewa na wageni watalii kutoka nchi za nje wanaofika kununua na kuhitaji maelezo ya kina kuhusu thamani ya bidhaa hizo.
``Sisi hapa sokoni tunakabiliwa na tatizo kubwa la kutozifahamu lugha za wenzetu, tunajitahidi angalau kuzungumza cha kuombea maji lakini wapi hatujafikia kiwango tunakariri tu. Jambo hili linatukoseshea sana wateja muhimu, serikali iliangalie tatizo letu,`` akasema Bw. Wales.
Wakasema lugha zinazowatatiza wafanyabiashara hao wawapo sokoni hapo ni za Kijerumani, Kirusi, Kifaransa, Kireno, Kiitaliano, Kispaniola na Kiingereza ambacho wanajitahidi kubahatisha maneno machache.
|