24 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakulima 50 Ilala kushiriki Nane Nane
 
2006-07-24 15:28:56
Na Mariam Mkumbaru, Jijini

Zaidi ya wakulima 50 kutoka Manispaa ya Ilala wanatarajiwa kushiriki katika maonyesho ya sikukuu ya wakulima ya Nane Nane ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika Arusha.

Kadhalika kampuni nne zimeonyesha nia ya kushiriki maonyesho hayo ambayo kikanda yatafanyika mkoani Morogoro.

Akizungumza na Alasiri ofisini kwake, Afisa Kilimo na Mifugo Dk.Andifas Sarimbo amesema wakulima hao wanatarajia kuonyesha mazao mbalimbali ya kilimo ambayo ni muhimu katika maisha ya kila siku.

Bw. Sarimbo katika maonyesha hayo watu watajionea namna ya kusindika mazao ya mifugo na kilimo, na jinsi ya kulima na jembe la mkono na la kukokotwa na ng\’ombe.

Kwa mujibu wa Bw. Sarimbo, maonyesho hayo yanatarajia kugharimu kiasi shilingi milioni 12.

Amesema pesa hizo ni kwa ajili ya maandalizi mbalimbali.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.