19 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ajali mbaya tena!
 
2006-07-19 14:48:07
Na Margareth Malisa, PST Kibaha

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine 43 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Pwani Shaibu Mohamed amesema ajali hiyo ilitokea juzi saa 12:00 jioni huko Rufiji eneo la Kinyanya.

Amesema ajali hiyo imehusisha Fuso lenye namba T 910 ACZ lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kwenda Kilwa.

Kwa mujibu wa Kamanda Shaibu, lori hilo lilikuwa na watu 77, uzito ambao anasema huenda ndiyo chanzo cha gari hilo kukosa mwelekeo.

Kamanda amesema gari hilo ni mali ya Bw. Mohamed Kinyama wa Kilwa Masoko ingawa amesema dereva aliyekuwa akiliendesha siku ya tukio hajafahamika.

Kamanda amewataja waliokufa kuwa ni Mapinduki Hassan, 32, mkazi wa Tabora, Hamisa Magani, 38 wa Manzese Jijini na Mbaraka Mussa, 20, mkazi wa Mbagala Jijini ambaye ni mwanafunzi wa Pwani Sekondari.

Wengine ni Said Makung\’ura mkazi wa Mbagala Jijini pamoja na Tausi Athumani ambaye alikuwa akielekea chuoni huko Mtwara alikokuwa akisomea Ualimu.

Kamanda amesema watu hao walikufa papo hapo na miili yao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Misheni Mchukwi iliyoko huko huko Rufiji.

Amesema majeruhi walikimbizwa katika hospitali hiyo kwa matibabu lakini 33 wakatibiwa na kuruhusiwa wakati kumi ambao hali zao ni mbaya wamelazwa.

Amewataja waliolazwa kuwa ni Azizi Hamid, 22, mkazi wa Lindi, Amida Kasembe, 21, mkazi wa Buguruni,Tijo Haji, 27, mkazi wa Lindi, Anastazia Michael, 25, mkazi Lindi na Kasembe Khalidi, 21, mkazi wa Buguruni.

Wengine ni Twaha Abdallah,22, mkazi wa Lindi, Abdul Raymond, 24, mkazi wa Mtwara, Shabani Mohamed, 24, mkazi wa Lindi na Yusuph Nasil, 50, mkazi wa Lindi.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.