17 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

DOWUTA wamfagilia Kikwete
 
2006-07-17 14:40:49
Na Zainab Kihate,Jijini

Chama cha wafanyakazi wa shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA), kimempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuteua Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA).

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Edmund Njowoka alipokuwa akizungumza na gazeti hili ofisini kwake.

”Kwa niaba ya wafanyakazi na wanachama wote wa DOWUTA, tunaipongeza serikali kwa kutuletea Mkurugenzi Mkuu, kwani tuna imani naye na tunaamini atashirikiana na chama chetu kuleta ufanisi na tija hapa TPA,” akasema
Bw. Njowoka.

Amesema Mkurugenzi huyo aliyeteuliwa alikuwa ni mfanyakazi wa siku nyingi katika bandari hiyo hivyo anaelewa vilivyo raha na kero katika taasisi hiyo nyeti na jicho la uchumi wa nchi.

Rais Kikwete hivi karibuni alimteua Bw. Ephraimu Mgawe, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, kuchukua nafasi ya Bw. Samson Luhigo aliyestaafu.

Bw. Njowoka alimuomba Mkurugenzi huyo kujipanga vizuri na timu yake na kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba DOWUTA itampa ushirikiano wa kutosha.

”Ufanisi wa kazi yoyote utaleta tija...kama hakuna mvutano kati chama cha wafanyakazi na Menejimenti lazima kazi zitafanyika kwa nguvu...taasisi itafikia malengo yake na wafanyakazi watapata stahili zao kwa wakati,” akasema Bw. Njowoka.

Akiongelea mkataba wa hiari wa wafanyakazi uliosainiwa hivi karibuni ukiwa ni mkataba wa kwanza toka Mamlaka hiyo ianzishwe, alisema umeanza kufanya kazi ambapo wafanyakazi waliostaafu wamepewa tuzo zao.

”Mkataba unasema wafanyakazi watakao ondoka kwa kustaafu kwa umri, ugonjwa au kufariki katika kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe ya kusainiwa mkataba huu, tuzo maalum ya kutambua mchango wao itatolewa na tayari tumeitoa,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa mkataba huo wanashughulikia malipo ya zamu za usiku ambazo wafanyakazi walikuwa wanadai kwa muda mrefu na kwamba zitalipwa wakati wowote.

”Nawaomba wafanyakazi watulie DOWUTA inapigania maslahi yao na sasa wanaodai malipo ya zamu za usiku wakati wowote wataanza kulipwa,” akasema Bw. Njowoka.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.