|
Moto wateketeza nyumba Kurasini
2006-07-14 15:52:10
Na Usu-Emma Sindila, Polisi Kati.
Moto mkubwa umetekateza nyumba na mali iliyokuwemo katika maeneo ya Kurasini Rungwe Jijini.
Akizungumza na Alasiri, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana amesema moto huo ulianzia kwenye chumba cha mpangaji mmoja wa nyumba hiyo, Doto Masoud, 33, almaarufu Mzige.
Amesema nyumba hiyo ni mali ya Bw. Athuman Hussein,35, almaarufu kama Kamtupe na ina vyumba kumi.
Amefafanua kuwa vyumba saba kati ya hivyo kumi, vilishika moto na kuteketea pamoja na mali iliyokuwemo.
Hata hivyo Kamanda hakusema thamani ya mali iliyoteketea wala chanzo cha moto huo.
Katika tukio jingine mkazi wa Jangwani Juma Omar, 30 ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na robo kilo ya mihadarati aina ya bangi.
Kamanda amesema Juma alitiwa mbaroni kufuatia msako wa polisi uliofanyika katika eneo hilo jana mchana.
|