Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Madereva wa daladala wagoma Moshi

16th June 2012
Print
Comments
Daladala

Madereva wa magari yanayofanya safari zake kati ya Pasua na kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi, wamegoma kuendelea kutoa huduma

kutokana na madai ya kunyanyaswa na Polisi wa Usalama barabarani na kutakiwa kutoa rushwa.

Mwenyekiti wa Madereva wanaofanya safari hizo, Joseph Lumwe, katika eneo la TBL, alisema kumekuwa na gari la polisi linalofanya doria, ambalo huwataka madereva kutoa Sh. 10,000 hadi 20,000 pamoja na kutoa kiasi hicho wanaendelea kukamatwa.

Hakuna gari ambalo ni zima kabisa, magari mengine mabovu na yameachwa kuendelea kutoa huduma, hakuna asiyejua magari ya eneo la Kahe, Weruweru, Soweto na Majengo kwa Mtei, nayo yanafanana na ya eneo la Pasua lakini ya eneo hilo yamekuwa yakikamatwa zaidi.

Alisema mara kadhaa wamekutana nao na kuzungumza juu ya suala hilo baina ya viongozi wa madereva hao na maofisa wa Jeshi la Polisi,

lakini hakuna mafanikio, jambo ambalo limesababisha wao kuendelea kuteseka. Lumwe alisema miundombinu mingi ya maeneo hayo ni mibovu sana, jambo ambalo linawafanya wamiliki wa mabasi kushindwa kupeleka magari yao mapya kwa ajili ya kutoa huduma hizo.

Leo tu wamekamata magari nane, mara nyingine unakamatwa na kufikishwa kituo cha polisi unaambiwa malipo ya makosa yote ni Sh. 120,000 lakini kwa kupitia mlango wa nyuma unaambiwa utoe Sh. 60,000 na

unaachiwa, hii si sawa, wanakamata magari yetu na kung’oa namba za usajili na wakati mwingine wanafanya hivyo maeneo ya barabarani au hata wakikuta magari yameegeshwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Kilimanjaro (RCO), Ramadhani Ng’anzi, alisema madai hayo hayana msingi kwani magari yote yanayokamatwa ni yenye makosa ikiwemo mabovu.

Alisema magari hayo yanakamatwa kutokana na operesheni ya mkoa mzima inayofanywa na jeshi hilo katika kuzuia madawa ya kulevya, ujambazi, makosa ya usalama barabarani, ambapo operesheni hiyo imeweza kukamata watu na vitu mbalimbali yakiwemo magari.

Ng’anzi alisema kwenye operesheni hiyo, lita 60 za gongo zilikamatwa na watuhumiwa 13, ambao watafikishwa mahakamani hivi karibuni, bangi kilo 3.5 na watuhumiwa nane, mirungi kilo 25 na watuhumiwa 17, konyagi feki katoni 60, majambazi sugu watatu na makosa ya barabarani 205 ambayo yalitozwa faini ya shilingi milioni sita.

Hata hivyo, aliwataka madereva wenye ushahidi wa kutoa rushwa au wanaoombwa rushwa na askari kunakili namba zao na kuzifikisha sehemu husika kwani kutoa na kupokea rushwa ni kosa kisheria.

 


 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment