Saturday May 18, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mwanajeshi kizimbani akidaiwa kubaka

21st July 2012
Print
Comments

Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Said Jumanne (32) amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kigoma kwa kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15 na kumpa ujauzito.

Mshtakiwa huyo alifikishwa jana mbele ya Hakimu  Mfawidhi wa Mahakama hiyo, David Ngunyale.

Aliposomewa shtaka lake alikana na yuko nje kwa dhamana ya wadhamini wawili waliowasilisha barua kutoka kwa mwajili wao na mali isiyohamishika yenye thamani ya Shilingi milioni moja.

Mwendesha Mashtaka wa polisi alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Awali akisoma hati ya mashtaka Inspekta wa polisi Alphonce Bandya, alidai kuwa Machi 28, mwaka huu majira ya saa 4 usiku huko Mwanga katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji mshtakiwa alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 15 na kumpatia ujauzito.

Hakimu Ngunyale aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 30, mwaka huu itakapo tajwa tena.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment