Sunday May 26, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Ujio wa Maximo sasa siri Yanga

16th June 2012
Print
Comments
Marcio Maximo

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwa sasa umeamua kufanya siri suala la ujio wa kocha wa zamani wa Taifa Stars, Marcio Maximo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Afisa Habari wa klabu hiyo, Luis Sendeu alisema uongozi umeamua kufanya hivyo baada ya kugundua kuna njama zinazofanywa na baadhi ya watu za kutuma taarifa za uongo kwa kocha huyo.

Sendeu alisema kuwa wapo baadhi ya wanachama wa klabu nyingine ambao wamemtumia barua pepe kocha huyo na kumpa taarifa kuwa kuna mgogoro mkubwa klabuni hapo.

"Lengo lao ni kutualibia mipango yetu baada ya kusikia kuwa tunamchukua Maximo... sasa suala la ujio wake  tutafanya siri kati yetu na Maximo ili kuepuka maneno ya watu," alisema Sendeu.

Alisema kuwa mipango yao na kocha huyo inaendelea na mambo yatakapokamilika atawasili nchini kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo.

Awali, mmoja wa wanachama wa klabu hiyo anayehusiska zaidi kwenye usajili Seif Ahmed 'Seif Magari' alinukuliwa akisema wapo baadhi ya waandishi wa habari wanaotumika kwenye hujuma hiyo.



SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment