



Benki ya CRDB imeanzisha utaratibu wa kutoa taarifa zake za kila mwezi kwa wateja kupitia njia ya barua pepe badala ya kutumia njia ya posta.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Tully Mwambapa, alisema huduma hiyo itarahisisha wateja kupata taarifa zao kwa haraka popote walipo.
“Huduma hii itawasaidia wateja wetu hasa wafanyabiashara kupata taarifa zao za kila mwezi kwa njia ya barua pepe ambayo itawawezesha kufungua anuani zao popote walipo na kuendeleza shughuli zao kwa urahisi zaidi na itasaidia utunzaji mazingira na kwa wale ambao hawana anuani za barua pepe wataendelea kupokea kwa njia ya posta” alisema Mwambapa.