Wednesday May 22, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Dk. Mgimwa ajivunia bajeti ya 2012/13

25th June 2012
Print
Comments
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa

Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa, amesema sensa ya Agosti mwaka huu ndicho  kipimo kitakachotumika kupima mafanikio ya Tanzania kwenye kutekeleza Malengo ya Milenia  (MDGs) ya Umoja wa Mataifa.

Dk. Mgimwa alisema hayo wakati wa ufunguzi wa  mafunzo ya wakufunzi wa sensa ngazi ya taifa  kutoka Bara na Visiwani yaliyoanza juzi  mjini Dodoma na kuongeza kuwa itatoa viasharia iwapo  Tanzania imetimiza MDGs  ifikapo 2015.

Malengo hayo ni pamoja  kuondoa umaskini kwa asilimia 50, kupunguza vifo vya wazazi na watoto wachanga, kumaliza njaa, kuleta usawa wa kijinsia, kudhibiti maambukizi ya VVU na kutunza mazingira.

Alisema takwimu hizo pamoja na kuwezesha kujulikana idadi kamili ya  watu, elimu, ndoa, umri, vifo, vizazi  na ajira zitawezesha kutathmini hali na ubora wa maisha ya wananchi na kupanga mikakati ya maendeleo endelevu.

Waziri Mkuu , Mizengo Pinda, akifungua mafunzo hayo, alisisitiza kuwa kutokana na umuhimu wa sensa kwa maendeleo ya taifa ni lazima  viongozi wote wa dini, siasa na asasi za kiraia watoe ushirikano wa dhati ili kufanikisha zoezi hilo.

Pinda, amewataka viongozi wote  kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa  sensa ya watu na makazi na kuhakikisha kuwa Watanzania wanashiriki na kutoa taarifa sahihi.

Aidha aliwataka Watanzania   kutunza kumbukumbu za taarifa za maswali yatakayo ulizwa kwa watu wote watakaokuwa wame lala kwenye kaya usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu ambayo ndiyo siku ya sensa.





 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment