Monday May 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

‘Walionizushia walilenga kunichafua’

26th June 2012
Print
Comments
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, ameingia bungeni kwa mbwembwe huku akisema waliosema kuwa amekamatwa ugoni mkoani Singida, walilenga kumchafua.

Kabla ya kujibu swali la Mbunge wa Pangani (CCM), Saleh Pamba, Simbachawene alipofika sehemu ya kujibia swali alinyoosha mikono yote miwi huku akitabasamu kwa furaha.

Wakati akinyoosha mikono juu, Bunge lililipuka kwa kukupiga makofi, hali iliyomfanya kuendelea kunyoosha mikono kwa muda huku akigeuka sehemu zote za ukumbi wa Bunge.

Hata hivyo, Spika Anna Makinda, alisema huko ni kupoteza muda kwa kushangilia.

Baada ya hali kutulia, Simbachawene alisema kulitokea uzushi kuwa amekatwa mkono.

Aliwataka Watanzania na wananchi wa jimbo lake la Kibakwe, kufahamu kuwa huo ni uongo uliokuwa unalenga kumchafua.

Baada ya maelezo hayo Simbachawene alianza kujibu swali la msingi, Pamba alitaka kufahamu matokeo ya utafiti wa mafuta ya gesi katika eneo la Makarawe Wilayani Pangani ambayo yalifanywa na kampuni ya Amoco miaka 1990.

Akijibu swali hilo, Simbachawene, alisema kampuni ya Amoco haikuwahi kufanya utafutaji wa mafuta katika sehemu za mikoa ya Tanga isipokuwa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kwa kushirikiana na kampuni ya Energy Development Corporation (IEDC), ya Kuwait.

Alisema TPDC na IEDC walifanya utafiti eneo hilo ambapo kisima cha utafutaji wa mafuta kilichimbwa katika eneo la Makarawe Wilaya ya Pangani mkoani Tanga mwaka 1984.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment