Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Cheka, Kaseba kuchangia ujenzi wa mabweni

25th June 2012
Print
Comments
Bondia Japhet Kaseba

Mabondia Francis Cheka na Japhet Kaseba watachangia harakati za ujenzi wa mabweni nchini kutokana na sehemu ya mapato yatakayopatikana katika pambano lao ‘kali’ litakalofanyika Julai 7 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imeelezwa.

Mmoja wa waratibu wa shindano hilo, Eric Shigongo, alisema kuwa asilimia 20 ya fedha zitakazopatikana katika tamasha liitwalo ‘Usiku wa Tumaini’, ambalo ndilo litakalowakutanisha Cheka na Kaseba, itapelekwa kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania ili kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike nchini.

Cheka na Kaseba ambao wamekuwa wakitambiana kwa wiki kadhaa sasa, wanatarajiwa kumaliza ubishi siku hiyo.

Cheka kutoka Morogoro, maarufu kwa jina la utani la ‘SMG’ atataka kuendeleza ubabe dhidi ya mpinzani wake huku Kaseba akitaka kulipiza kisasi baada ya kupigwa vibaya katika pambano walilokutabna kwa mara ya mwisho.

Kwa mujibu wa waandaaji, tamasha la ‘Usiku wa Tumaini’ litaambatana pia na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na muziki kutoka kwa nyota wa bongofleva, Diamond na Jose Chamaleon kutoka Uganda.

Kutakuwa pia na mapambano yab soka baina ya mashabiki wa klabu za Simba na Yanga, wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasanii wa bongofleva watavaana na wasanii wa filamu (Bongo Movie).

 “Usiku wa Tumaini hauna malengo ya kisiasa, shabaha yake ni kuchochea tumaini jipya kwa kuwaweka pamoja Watanzania wa kada mbalimbali ili kuburudika kwa michezo, sanaa za aina tofauti kama vile muziki, maigizo, vichekesho na pia kuliombea taifa lao,” ilielezwa.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment