Thursday May 23, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Sugu: Tujitoe kushiriki kimataifa

26th June 2012
Print
Comments
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema)

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), ameitaka serikali kusitisha ushiriki wa timu za taifa za michezo mbalimbali katika mashindano ya kimataifa hadi hapo kutakapokuwa na maandalizi ya kutosha.

Mbilinyi aliyasema hayo wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza, akiuliza, "ni kwa nini serikali isisitishe kushiriki katika mashindano ya kimataifa kwa kuwa timu hazifanyi vizuri hadi hapo zitakapokuwa tayari?"

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla alisema si vema kwa serikali kusitisha timu zisishiriki katika mashindano hayo.

Alisema kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa kunaitangaza Tanzania pamoja na vivutio vyake.

“Timu kufanya vibaya ni jambo la kawaida, sioni kama tukiacha kushiriki ndiyo tutaendelea kufanya vizuri…hivyo ni bora kushiriki ili tuone wapi tumekosea,” alisema

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Ziwani, Ahmed Juma Ngwali (CUF), alitaka kujua serikali kupitia Kamati ya Olimpiki  Tanzania (TOC), inakusudia kupeleka washiriki wangapi kuiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki  itakayofanyika London nchini Uingereza.

Akijibu swali hilo, Makalla alisema Tanzania itawakilishwa na jumla ya wachezaji sita katika mashindano hayo yatakayofanyika Julai hadi Agosti mwaka huu.

Alisema kati ya wachezaji hao, wanne watashiri katika mchezo wa riadha, mmoja mchezo wa ngumi na mwingine kuogelea.

Alisema timu hiyo itakuwa na makocha wanne, ambapo wawili watakuwa wa mchezo wa ngumi, mmoja wa kuogelea na mwingine wa riadha.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment