Sunday May 26, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

JK aunga mkono AfDB kurudi Ivory Coast

2nd June 2012
Print
Comments
Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete ameunga mkono ombi la Serikali ya Ivory Coast ya kutaka kurejeshwa makao makuu ya benki ya maendeleo ya Afrika, AfBD nchini humo kutokana na kumalizika kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ilisababisha makao makuu ya benki hiyo kuhamishiwa nchini Tunisia.

Rais Kikwete, alitoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro mara baada ya kumuaga Rais Allassane Ouattara wa Senegal, aliyekuwa mjini Arusha akihudhuria mkutano mkuu wa magavana wa benki ya maendeleo barani Afrika.

Akijibu maswali ya waandishi habari, Rais Kikwete, amesema kuwa makao makuu ya benki hiyo yalihamishwa nchini  Ivory Coast, kutokana na machafuko yaliyotokea lakini tayari amani imesharejea hivyo hakuna sababu ya makao makuu ya benki hiyo kuendelea kuwepo nchini Tunisia.

Rais Kikwete ameishukuru benki hiyo kwa kuleta mkutano huo mkubwa hapa nchini ambao unafanyika kwa mara ya kwanza tangu benki hiyo ianzishwe miaka 47 iliyopita na kusema kuwa hiyo ni heshima kwa Tanzania.

Akizungumza kwa lugha ya Kifaransa, katika mkutano wa ufunguzi, rais wa Allassane Outtara, aliiomba wajumbe wa mkutano huo kukubali kurejeshwa makao makuu ya benki hiyo nchini kwake kwa kuwa amani imesharejea na hivyo kazi zitafanyika kwa ufanisi.

Outtara, amesema hakuna haja ya makao makuu ya benki hiyo kuendelea kubakia nchini Tunisia, hivyo akawaomba waangalie uwezekano wa kurejesha makao makuu nchini mwake .

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment