Saturday May 18, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Tucta na bajeti

21st June 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya

Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Nchini (Tucta), limesema bajeti ya serikali ya mwaka 2012/2013 haina jipya linalolenga kuwakomboa wafanyakazi na kutatua kero zao za muda mrefu kuhusiana na ugumu wa maisha.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya, iliwaomba wabunge kusimama imara wakati wa kujadili bajeti hiyo huku wakiangalia wananchi hususani waliopo vijijini.

Mgaya alisema serikali inapaswa kuangalia zaidi kukuza kipato cha mwananchi wa kawaida kuliko kutazama ongezeko la pato la taifa ili kuhakikisha maisha ya wananchi yanaboreshwa na kuwaondolea ugumu wa maisha.

Alisema kukuza pato la taifa pekee hakutoi picha halisi ya maisha ya Watanzania na badala yake kunaongeza mapato ya watu matajiri wanaomiliki makampuni makubwa ya biashara.

Kuhusu mishahara, Mgaya alisema bado ni midogo na isiyokidhi mahitaji muhimu ya maisha yakiwemo ya chakula, elimu, matibabu, mavazi, malazi pamoja na huduma za maji na nishati.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment