Tuesday May 21, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Kesi za ardhi kumalizika miezi 3

6th July 2012
Print
Comments

Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, imeandaa program maalumu ya miezi mitatu kwa ajili ya kusikiliza mashauri  600 kati ya 1,912 yaliyoko katika mahakama hiyo itakayowahusisha majaji wote 10 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni.

Programu hiyo itasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa mlundikano wa kesi uliokuwa unasababishwa na upungufu wa majaji.

Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Ardhi, Agathon Nchimbi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari .

Jaji Nchimbi alisema kwamba kesi zitakazohusika katika zoezi hilo ni za rufaa, maombi na mapitio na hivyo akawaomba wananchi wenye mashauri yao kuwasiliana na msajili wa mahakama hiyo kuanzia Julai 9, mwaka huu ili kujua kama kesi zao zimo au kwa maelekezo zaidi.

“Majaji wote 10 walioteuliwa na rais wameletwa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi , kabla hawajapangiwa maeneo mengine ya kwenda kufanyia kazi na kwa hali hiyo tukaona tuwatumie katika program hii ili wasikilize mashauri hayo na kuyaamua,katika kipindi hicho tulichokiweka” alisema
.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment