Saturday May 18, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Kaseja aota ubingwa Kagame

21st June 2012
Print
Comments
Nahodha wa Simba na timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Juma Kaseja

Nahodha wa Simba na timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Juma Kaseja, amesema kuwa baada ya kurejea nchini juzi akitokea Msumbuji, sasa akili yake anaielekeza katika kuisaidia klabu yake ili itemize lengo la kutwaa taji la michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14 hadi 29.

Akizungumza na NIPASHE, Kaseja aliyepangua penati mbili katika mechi ambayo Stars walifungwa na Msumbiji kwa ‘matuta’, 7-6, alisema kuwa amekubaliana na matokeo waliyopata na sasa kilichobaki ni kwa yeye na wenzake kujipanga upya kwa ajili ya kuzitumikia vyema timu zao.

Kaseja na nyota wengine wa Stars wakiwemo 10 wa klabu ya Simba walirejea nchini juzi usiku. Kipa huyo na wenzake wa Simba wanatarajiwa kuungana na kikosi chao katika mazoezi ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ yanayoendelea kwenye viwanja vya Sigara (TCC), Chang'ombe.

Katika hatua nyingine, imefahamika kuwa Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara watajipima nguvu Jumapili kwa kucheza dhidi ya Express ya Uganda kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment