Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Dk. Mengi: Waandishi fanyeni kazi kwa uzalendo

22nd July 2012
Print
Comments

Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) Dk. Reginald Mengi amewataka waandishi wa habari nchini kufanya kazi kwa uzalendo kwa kuandika habari zenye kujenga.

Dk. Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, alisema hayo wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mhariri Mwandamizi wa gazeti la East Africa kwa upande wa habari za biashara, James Mwakisyala (64), yaliyofanyika jana eneo la Pugu Kinyamwezi jijini Dar es Salaam.

Alisema binafsi alimfahamu marememu Mwakisyala kama rafiki yake na mara nyingi alikuwa anapenda tabia yake ya ufanyaji kazi kwa kufuata haki, maadili na kujenga kamwe hakuandika habari zake kwa kutaka kubomoa jamii.

Aliwataka waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini kuuenzi mchango wa marehemu kwa kufuata nyayo zake kwa kufanyakazi kwa weledi na kuweka maslahi ya umma mbele kuliko maslahi binafsi.

"Kuna jambo moja nimejifunza kwa rafiki yangu James, naomba waandishi pia wanielewe kwa umakini kuwa katika utendaji wake wa kazi alikuwa tofauti sana, alifuata wajibu na hakutaka kuandika kwa ajili ya kubomoa na mara zote alikuwa akijiuliza kabla ya kuandika kwa ajili ya maslahi ya wengi," alisema Dk. Mengi.

Dk. Mengi aliahidi kumsomesha mtoto mdogo wa marehemu Jacquline Mwakisyala (12) anayemaliza darasa la saba Shule ya Msingi Bunge mwaka huu kama moja ya kumuenzi na kuthamini mchango wake katika kipindi cha uhai wake.

Awali ibada ya mazishi iliendeshwa na nabii Amos Kazamura ambapo alieleza kifo ni moja ya njia ya kuelekea katika maisha mapya, hivyo hakuna sababu kwa familia na marafiki kusikitika sana kwa kuwa marehemu kabla na baada ya kifo chake alikuwa muumini mzuri na ana kila aina ya dalili ya kuwa karibu na Mungu.

Marehemu Mwakisyala alizaliwa mwaka 1948 Wilayani Rungwe na alipata elimu ya ngazi mbalimbali ikiwemo Shahada ya uandishi aliyopata nchini Canada mwaka 1971, aliporudi nchini alibahatika kufanya kazi Benki kuu kama Mkurugenzi wa mawasiliano na itifaki, magazeti ya The African, Daily News, Citezen na East Africa. Marehemu ameacha mke na watoto wanne.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment