Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mabalozi wamchangia Mama Maria Nyerere

21st June 2012
Print
Comments
Mama Maria Nyerere akiwa na umoja wa Mabalozi wa Afrika waliopo nchini walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam na kumkabidhi hundi ya dola 650 za Marekani kwa ajili ya taasisi yake ya kusaidia watoto yatima na wa mazingira magumu iliyopo Butiama mkoani Mara.

Mabalozi wa nchi za Afrika wanaoishi nchini wamekabidhi Sh. milioni 10.3 kwa mke wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Maria Nyerere, ukiwa ni mchango wao katika kusaidia kituo chake cha kusaidia watoto yatima na walemavu cha Butiama.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mchango huo myumbani kwake Msasani, jijini Dar es Salaam, kiongozi wa mabalozi hao, Balozi Ibrahim Mukubi wa Uganda, alisema wametambua na kuthamini mchango na juhudi za Mama Nyerere katika kusaidia watoto yatima na walemavu, hivyo kuamua kumuunga mkono kwa mchango huo.

“Katika kipindi cha maadhimisho ya miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania, sisi kama mabalozi tulitembelea Butiama na tukaona juhudi za mama katika kusaidia watoto, hivyo tukaona na sisi tumuunge mkono katika kazi yake hiyo,” alisema Balozi Mukubi.

Balozi wa Kenya nchini, Mutinda Mutiso, alisema tatizo la watoto wa mtaani ni kubwa katika bara lote la Afrika kutokana na kukosekana kwa amani na kwamba iwapo amani itapatikana katika nchi zote, tatizo hili litakwisha kabisa.

Alisema serikali katika nchi zote za Afrika zimekuwa zikitekeleza mikakati mabalimbali katika kutatua tatizo hilo na kwamba wao wamefanya sehemu ndogo tu ya kusaidia tatizo hilo.



 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment