Thursday May 23, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Bayi aendelea kuitangaza nchi

30th June 2012
Print
Comments
Katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi

Katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi ametunukiwa tuzo ya mwanariadha bora wa zamani wa Afrika aliyeliletea sifa taifa, baada ya kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya mchezo huo  ya Afrika yaliyofanyika Lagosi Nigeria 1973.

Tuzo hizo zilitolewa Jumatatu nchini Benin na Shirikisho la Riadha Barani Afrika (CAA) wakati wa mashindano ya riadha ya kuwania ubingwa wa Afrika yanayoendelea nchini humo. Katika mashindano hayo ya 1973 Bayi alitwaa medali hiyo katika mbio za mita 1,500 na kutumia muda wa 3:37:2, na kufanikiwa kutwaa medali ya dhahabu Nigeria.

Mbali na medali hiyo pia Bayi amepata tuzo hiyo baada ya kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za mita 1500 kwenye mashindano ya Jumuiya ya madola yaliyofanyika Christchurch, New Zealand mwaka 1974 baada ya kutumia muda wa dakika 3:32.2.

Katibu huyo alivunja rekodi ya dunia mwaka 1975, Kingston Jamaica katika mashindano ya mwaliko ya maili moja, baada ya kutumia muda wa 3:51.0, na baadae alipata medali ya dhahabu mwaka 1978 Algiers Algeria katika mashindano ya Afrika.

Bayi alisema medali nyingine aliyoipata ni ya fedha katika mita 1,500 kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Edmonton Canada baada ya kutumia muda wa 3:34.5.

Alisema medali nyingine iliopelekea kupata tuzo hiyo ya CAA ni ile ya fedha aliyoipata katika mchezo wa kuruka magongo ambapo alitumia dakika 8:12.5, katika mashindano ya michezo ya Olimopiki yaliyofanyika Moscow, Urusi mwaka 1980.

Alisema sababu ya kupewa tuzo hizo pamoja na medali ni kutokana na wanariadha hao kuliletea sifa taifa katika mashindano mbali mbali ya kimataifa kwa kutwaa medali.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment