


.jpg)
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma, jana waliungana na waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa mtumishi wa Ikulu, marehemu Deokalyus Makwasinga, nyumbani kwake Kimara-Kilungule, Dar es Salaam.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam ilieleza kwamba marehemu Makwasinga, ambaye alikuwa dereva wa miaka mingi Ikulu, alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia ajali mbaya ya gari eneo la Kimara-Korogwe, Msikitini, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita.
Mara baada ya shughuli ya kuaga, mwili wa marehemu Makwasinga, ulianza safari ya kupelekwa Mahenge mkoani Morogoro ambako atazikwa.
Marehemu ameacha mjane na watoto watatu.