Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Tuzo ya dhababu ya TBL yawasili

25th June 2012
Print
Comments
Mpishi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Gaudence Mkolwa (katikati) akipokea tuzo ya kimataifa ijulikanayo kama 'Grand Gold Award' kutoka kwa Meneja wa Bia ya Ndovu Special Mult, Pamela Kikuli (kulia) Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Habrai na Mawasiliano, Edith Mushi.

Tuzo ya dhahabu ya kimataifa iliyotwaliwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL), imewasili nchini na kupokelewa na meneja wa kinywaji kilichotwaa tuzo hiyo ya Ndovu Special Mult, Pamela Kikuli.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kikuli alisema kama kampuni wamefurahishwa na ushindi huo wa mara ya pili mfululizo na kusema tuzo hiyo imeiletea sifa nchi na kuitangaza kimataifa.

Akifafanua kuhusu tuzo hiyo, Kikuli alisema hiyo ni tuzo ya juu kabisa katika tuzo za bidhaa za kimataifa zinazotolewa na taasisi ya kimataifa inayoangalia ubora wa bidhaa ya ‘Monde Selection International Quality Institute' iliyopo Athens Ugiriki.

Tuzo hiyo ambayo kwa mara ya pili mfululizo inanyakuliwa na bia hiyo inajulikana kama "Grand Gold Award" na hushindanisha bidhaa kutoka mataifa mbalimbali, ambapo mwezi Aprili mwaka huu Ndovu Special Mult ilitangazwa kuwa mshindi na sasa ndio imewasili nchini.

Naye Mpishi Mkuu wa bia wa TBL, Gaudence Mkolwa, alisema wamefurahishwa sana na ushindi huo na sasa wako tayari na wanahaki ya kusheherekea kwa kupita wakiitembeza tuzo hiyo maeneo mbalimbali ili Watanzania wajivunie kilicho chao.

Akikabidhi tuzo hiyo, meneja wa wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Express, Busegi Kulwa, alisema kampuni yao inajiskia faraja sana kufanya kazi na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kutokana na mafanikio wanayo ya pata kimataifa.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment