Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mwakyembe: kujiuzulu si ufumbuzi wa kila tatizo

21st July 2012
Print
Comments
Waziri wa Uchunguzi, Dk Harrison Mwakembe

Utamaduni wa kujiuzulu si ufumbuzi wa  kila tatizo linapotokea katika jamii, Waziri wa Uchunguzi, Dk Harrison Mwakembe alisema mjini hapa jana.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari  juu ya uwezekano wa viongozi wa Zanzibar kuwajibika kwa ajali ya MV Skajit, Dk Mwakyembe alisema shikizo hilo ni mapema mno.

Alisema taarifa za awali juu ya tukio hilo lililosababisha watu wengi kupoteza maisha zinaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni hali mbaya ya hewa.

Katika mkutano huo mawaziri watano, wakiwemo watatu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na wawili wa serikali ya Muungano walijibu maswali mbali mbali likiwemo lililogusa uwezekano wa kujiuzulu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano  Zanzibar,  Hamad Masoud.

Kabla ya Waziri  Masoud kujibu swali hilo, Dk Mwakyembe, ambaye kwa taaluma ni mwanasheria alisema, “naomba nizungumze kidogo, jibu litatolewa maelezo zaidi na mheshimiwa waziri – Masoud.”

Dk Mwakyembe alisema shinikizo la kumtaka Waziri Masoud kujiuzulu ni mapema mno, hasa kwa kuzingatia maelezo kwamba dalili za kuwa na hali ya hewa mbaya hazikuonekana hadi ilipotokea.

Alisema wataalam wa mamlaka ya hali ya hewa wametoa maelezo kwamba chanzo cha cha ajali ni upepo na kwamba chombo hicho hakikuwa na tatizo lolote wakati kinaanza safari Dar es Salaam.

“Sidhani kama kujiuzuli ni solution kwa kila tatizo,…ajiuzulu kwa sababu upepo umetokea!,” aliongeza  Dk  Mwakyembe.
Mapema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhiti wa usafiri wa majini na nchi kavu (Sumatra), Ahmad Kilima, alisema meli hiyo ilifanyiwa ukaguzi kabla ya safari na kuthibitika haikuwa na tatizo lolote la kiufundi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mawaziri hao mpaka sasa watu 68  wamepoteza maisha katika ajali hiyo na wengine wapatao 150 waliokolewa.

Dk Amed Makata, mtaalam wa masuala ya uchunguzi wa vifo na utambuzi wa makao makuu ya polisi alisema katika mahojiano kwamba watu 10 kati ya waliopoteza maisha hadi jana asubihi walikuwa bado hawajatambuliwa hadi jana asubuhi.

Alisema kati ya maiti hao, tisa ni wanawake na mwanaume moja,  raia wa kigeni . “Tunafanya uchunguzi wa vinasaba ili kujua uraia wake,” alisema Dk Makata.

Dk Makata alisema kwa kawaida zoezi la uokozi linatazidi kuendelea kulingana na kuendelea kupatikana maiti, japokuwa kituo cha utambuzi wa watu waliokufa cha Maisara kinaweza kusitisha operesheni zake.


 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment