Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Pinda leo kuwasilisha bajeti ya ofisi yake

25th June 2012
Print
Comments
Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Baada ya mapumziko ya mwisho wa wiki, leo wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano ya Bunge, ofisi hiyo itajadiliwa kwa siku tano.

Ofisi ya Waziri Mkuu inajumuisha Sera, Uratibu na Bunge; Uwekezaji na Uwezeshaji pamoja na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Mjadala mkali unatarajiwa kuibuka wakati ya bajeti ya Tamisemi ambapo fedha nyingi za miradi ya maendeleo zinazopelekwa huko zimekuwa zikifujwa kwa muhinu wa Ripoti ya kila mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Pia wabunge wamekuwa wakilalamika kwa fedha zilizoidhinishwa na Bunge hazikupelekwa zote na hivyo miradi mingi kushindwa kukamilika kwa wakati. Wiki iliyopita wabunge walijadili na kupitisha, bajeti ya mwaka 2012/13 ambapo Sh. Trilioni 15 zimeidhinishwa.

Bajeti ya maendeleo ilipangiwa asilimia 30 ya bajeti nzima (sawa na Sh trioni 4.5), jambo ambalo lilizua mjadala kutoka kwa wabunge kuwa haiendani na  Mpango wa Maendeleo wa Taifa.

Mjadala mkali uliibuka huku baadhi ya wabunge wakiwemo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakitishia kuipinga bajeti hiyo, hali iliyoilazimu kufanyika kwa vikao vingi vya wabunge wa CCM na pamoja na vya mawaziri kuhakikisha bajeti hiyo inapitishwa.

Miongoni mwa wabunge hao ni Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina, ambaye hata wakati wa kupiga kura, aliondoka ndani ya ukumbi wa Bunge.



 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment